Crictiano Ronaldo ameziweka klabu za Manchester City, United, PSG, Chelsea katika hali ya kujitayarisha kuingia vitani ili kumpata baada ya kuthibtisha anataka kuondoka Real Madrid.
Mtu wa karibu yake alipoulizwa alisema: "Kweli, Cristiano amemwambia Raisi Florentino Perez anataka kuondoka klabuni hapa."
Hayo
yamekuja baada ya Ronaldo,27, kufunga goli mbili siku ya Jumapili
lakini hakushangilia goli lolote katika hayo mawili dhidi ya Granada.
Na alipulizwa baada ya mechi alisema: "Nina huzuni na viongozi wa klabu wanajua.
"Ni mambo ya kitaaluma (Professional Issue). Siwezi sema zaidi ya hapo."
Ronaldo akiwasili kwenye kambi ya mazoezi ya Real jana Jumatatu |
Ronaldo
ana kifungu katika mkataba wake(release clause) ambacho kinamruhusu
kuondoka klabuni hapo kama timu itaweza kuilipa Real pauni milioni 100 (Real wanadai ni zaidi ya pauni milioni 700) na kuweza kumlipa mshahara utakaoanzia pauni 25,000 na kuendelea kwa
wiki.
Kwa wakati huu kuna timu chache ambazo zinaweza kufanya hivyo: Manchester City au PSG, na hata Chelsea.
Jose
Mourinho pia hatarajiwi kuwepo Real muda mrefu ujao, kuna uwezekano akaondoka majira ya joto yajayo na atapendelea kuondoka na Ronaldo kama
ataenda timu zenye fedha za kumwaga kama City au PSG.
Akisindikizwa kama ilivyo ada kwa wachezaji wote wanapowasili mazoezini |
Cristiano
alinunuliwa kutoka Manchester United mwaka 2009 kwa ada ya pauni
milioni 80, akiwaongoza Real vema kuchukua vikombe msimu uliopita akifunga
mabao 46 katika michezo 38 ya La Liga na jumla ya mabao 60 katika
mashindano yote aliyoichezea Real - kitu kinachomfanya afikirie labda
anatakiwa kuongezewa mshahara.
Ameshaifungia Real Madrid jumla ya magoli 150 akiwa na wastani wa goli zaidi ya moja kwa mechi lakini kwa Spain, Messi ndiye anayeonekana bora.
Kuna wanasema kitendo cha Messi kuonekana ni bora zaidi yake huwa kinamnyong'onyesha sana.
Hichi ndicho alichoweza kufanya baada ya kushindwa kushangilia goli la pili kwa kua hana furaha kuwepo Madrid |
Ronaldo hathaminiwi kama ambavyo Messi anavyotukuzwa Barcelona na kituo kimoja cha radio kiliripoti kwamba Ronaldo amemuambia Raisi wa Real kwamba hata katika vyumba vya kubadilishia nguo (Dressing Room) Real Madrid hathaminiki.
Akihudumiwa baada ya kujeruhiwa katika mechi dhidi ya Granada |
KAZI NJEMA!!!!!!!.
No comments:
Post a Comment