Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amempa Theo Walcott masaa 48 kuanzia sasa kuamua kama atasaini mkataba wa miaka mitano kwa malipo ya pauni 75,000 kwa wiki au kuuzwa.
Theo yupo mazungumzoni na Arsenal ila uwezekano wa kubaki ni mdogo |
Kama Theo akikataa kusaini mkataba - kuna chaguo moja kati ya mawili Arsenal wanatakiwa kuchagua - kumuuza sasa ama kuhatarisha aondoke bure majira ya joto ya usajili yanayofuata.
Theo yupo mazungumzoni na Arsenal ila uwezekano wa kubaki ni mdogo |
Walcott yupo ndani ya miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na Arsenal, na bado hajatia saini ili kurefusha mkataba huo, ingawa mazungumzo yanaendelea inaonekana Walcott hatosaini mkataba huo.
Livepool na City wanasubiria kwa hamu kumnyakua |
Liverpool na City wako tayari kumnasa winga huyo iwapo hatotia saini.
Serge Gnabry: Mrithi wa nafasi ya Walcott iwapo ataondoka Emirates |
Wakati huu, Nicklas Bendtner yupo katika maongezi mazito na AC Milan juu ya uhamisho utaogharimu pauni milioni 5 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Ijumaa hii.
JUMATANO NJEMA!!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment