Jana iliripitiwa kwamba Cole alikua tayari ameamua kuihama timu hiyo bure majira ya joto yajayo baada ya kutokuridhishwa na muda wa mkataba aliokuwa aongezewe na Chelsea.
Inadaiwa Chelsea walimpa ofa Ashley Cole(31) ya kuongeza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa uliobakisha mwaka mmoja kumalizikia.
Ikizingatiwa kwamba kama Cole akikataa kusaini mkataba mpya aliobakiza mwaka mmoja tu, basi majira kama haya ya dirisha la usajili mwakani atakua huru kuondoka bure.
Cole akikwepa maswali ya waandishi wa habari jana
Mwezi uliopita A. Cole alipinga vikali habari zilizokua zimezagaa kwamba alikua nataka aongezewe mshahara kufikia pauni 200,000 kwa wiki.
Chelsea hawataki kumpoteza Cole, na hakuna ubishi kama ataamua kugoma kusaini basi kuna timu kubwa za Ulaya zitamgombea.
Amekua akihusishwa na kumfuata Mourihno Real Madrid, pia kuna timu nyingi watataka kumshawishi kwa kumtengea dau kubwa alitakalo.
SIKU NJEMA!!!!!!!!
|
No comments:
Post a Comment