Safari hii ni Bacary Sagna, ambaye anaishutumu timu hiyo kwa kuwauza Robin vab Persie na Alex Songi huko yeye mwenyewe akishindwa kuthibitisha kama ataendelea kuwepo klabuni hapo.
Sagna aliliambia gazeti la L'Equipe: 'Pindi wachezaji wenu wawili bora wanapoondoka, lazima utaanza jiuliza maswali.
'Kuna wakati mashabiki hunifuata na mtaani na kuniuliza, cha ajabu hata mimi mwenyewe sijui.
'Kila mtu alijua RVP angeondoka, lakini sio Song.
'Bado mdogo, ana miaka 24 na akiawa amebakiza miaka mitatu katika mkataba wake. Tumepoteza sana.
'Baada ya msimu huu kumalizika nitabakisha mwaka mmoja.'
Haijampendeza Sagna kuona Song anakwenda Barca |
Sagna kwa sasa anapokea pauni 60.000-kwa-wiki ila anatarajia kupata nyongeza ya mshahara kama atakubali kusaini mkataba mpya.
Hali hii kama Samir anavyoonekana ndio anayoitaka Sagna, makombe! |
SIKU NJEMA!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment