Luca Modric atatambulishwa kama mchezaji wa Real Madrid siku ya Jumatatu baada ya usajili wa pauni milioni 33 kukamilika leo.
Kiwango hicho ni pungufu ya kile walichokuwa wanataka Tottenham, ambacho ni zaidi ya pauni milioni 35.
Mambo poa: Modric akiwa katika uchunguzi wa afya kabla ya kutia saini |
Mara baada ya kumaliza kusaini mkataba na kuwa rasmi mchezaji wa Real |
Makubaliano ya Madrid na Spurs yalikuwa magumu kufikiwa kutokana na ada ya uhamisho waliyokuwa wanataka kulipa Real na kiasi walichokuwa wanataka kulipwa Tottenham.
Hivyo kupelekea kuingiwa kwa mkataba mwingine wa USHIRIKIANO kati ya klabu hizo mbili.
Akitabasamu baada ya kupima afya |
Akipozi kwa ajili ya picha |
Modric alifanikiwa kufaulu uchunguzi wa afya leo asubuhi, na baada ya taratibu wa kiofisi kukamilika atasaini mkatba wa miaka mitano wa kuwa Bernabeu.
Tovuti ya Real Madrid iliandika: "Mchezaji mpya wa Real Madric, Luka Modric amefaulu uchunguzi wa afya uliofanyika katika hospitali Sanitas La Moraleja kabla ya kusaini rasmi na klabu.
Modric amejiunga Real Madric akitokea Tottenham |
Tottenham sasa wana kazi ya kusaka mrithi wa Modric ikizingatiwa muda wa usajili uliobaki ni mdogo.
Mitego ya Spurs ipo kwa Wabrazili wawili: Willian anayechezea Shakhtar Donetsk na Leoandro Damiao Intanacional.
Wanted: Willian anatakiwa na Tottenham kupunguza machungu ya Modric |
Happy Monday!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment