Bosi wa Manchester United Alex Ferguson amewamepiga marufuku wachezaji chipukizi walio chini ya umri wa miaka 23 kuendesha magari ya kifahari kutoka kwa wadhamini wao wapya Chevrolet ama kununua mahali pengine.
Suala hilo limekuja baada ya kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari Chevrolet waliyoingia mkataba wa mamilioni na Manchester United hivi karibuni kutoa ofa kwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza.
Bosi Ferguson: Aingilia kati kulinda vijana wake |
Baada ya makubaliano ya udhamini wa kuvaa jezi zanye nembo ya Chevrolet kuanzia msimu wa mwaka 2014-2015, kampuni hiyo ilitoa ofa kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu kuchagua kila mmoja gari la kifahari kama shukrani kwa United.
Welbeck: Bado miaka 2 |
Jones: bado miaka mitatu |
.
Hapo Fergie akaingilia na kupiga marufuku kwa wachezaji wote chini ya umri wa miaka 23 kuwa mbali na magari hayo bila kujali umaarufu wao.
Hii inamaanisha kina Danny Welbeck 21, Phili Jones 20, Chris Smalling 22 na Rafael 22 hawataruhusiwa kuendesha gari lolote mpaka Ferguson awe ameliona na kulipitisha.
Ferguson hua makini na wachezaji wake na huhakikisha wachezaji wake hawavimbi kichwa kwa umaarufu na pesa nyingi walizokuwa nazo.
Kwa mfano miaka miwili iliyopita alikataza wachezaji wa timu B kuvaa viatu vya rangi za kung'aa.
NI marufuku kwa mchezaji wa timu ndogo kutia mguu kwenye viatu vyenye rangi kali.
JUMANNE NJEMA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment