City walidhani Maicon angewagharimu pesa nyingi wakati Inter walipowapa ofa ya kumnunua, mazungumzo yalikua rahisi na maafikiano yakafikiwa kwa haraka.
M-Brazili huyo wakati huu keshafika Uingereza kukamilisha usajili kamili.
Inaamimika Maicon mwenye umri wa miaka 31, atasaini mkataba wa miaka miwili huku akipokea mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki. Staa huyo wa Brazil hucheza kama winga mkabaji anayepanda na kushuka.
Na mchezaji De Jong wa City yupo katika jiji la Milan kuhitimisha kujiunga na AC Milan baada ya maombi yake ya kuongezewa mshahara kugonga ukuta na hivyo Mancini kuamua kumuuza kwa pauni 3.5 milioni.
De Jong: njiani kuelekea AC Milan
Mancini ameonelea anaweza asimtegemee sana
kiungo huyo mkabaji katika kampeni zake za kusaka makombe na ushirki wao katika Michuano ya Kombe La Klabu Bingwa Ulaya 2012/2013 huku wakiwa wamepangawa katika kundi gumu linalojumuisha mabingwa katika nchi zao Real Madrid akiwa ni bingwa wa Uhispania, Ajax ya Uholanzi na Mabingwa wa Ujerumani Borusia Dotmund.
ALJUMAA KAREEM.
|
No comments:
Post a Comment