Winga wa Manchester United ametishia kugoma kusaini mkataba United huku akisubiri muda wa mkataba huo uishe ili aondoke bure.
Nani amekasirishwa na kitendo cha United kumtoa sadaka kwa Zenit St. Petersburg ikiwa timu hiyo si chaguo lake.
Ili kukwamisha suala hilo Nani alitaja kiwango kikubwa cha mshahara ili kujiunga na timu hiyo ( zaidi ya pauni 200,000 kwa wiki) , akijua wazi watashindwa na hivyo kuachana nae.
Nani akiwa mazoezini na kikosi cha timu ya Taifa Portugal juzi mchana |
Chanzo cha habari cha klabu ya Zenit kilisema: ' Haikua bahati mbaya Nani kutokupatikana kwenye simu, Alimwambia ajenti wake ataje kiasi kikubwa cha pesa kama Zenit wanataka kuongea nae. Akitarajia itawavunja nguvu na kuachana nae ila zenit walikubali na kutaka waongee nae.
'Mwishowe, Nani alizima simu yake na kuwaambia watu aliokuwa nao wakiulizwa waseme hawajui alipo.'
Nani bado ana mkataba na United uliobakisha miaka miwili, na aliomba United wamuongezee mshahara japo kufikia pauni 130,0000-kwa-wiki kitu ambacho mpaka sasa United hawajaafiki,
Iwapo Man U wataendelea kukaza basi nae atatia ngumu ili mwisho wa mkataba wake aondoke bure na kuikosesha United zaidi ya pauni milioni 20 iwapo angeuzwa.
JUMAPILI NJEMA!!!!!!
No comments:
Post a Comment