Robin van Persie na mkewe Bouchra wakiwasili Rosso Restaurant |
ROBIN van Persie aliwasili jana jijini Manchester na usiku wa kwanza aliutumia katika mgahawa wa mchezaji mwenza Rio Ferdinand.
Mshambuliaji huyo, ambaye alizua gumzo kwa kukataa kuongeza mkataba Arsenal na kutimkia Manchester United wiki hii, alionekana akiwasili kwa chakula cha jioni katika mgahawa wa Rio uitwao Rosso.
Robin, 29 aliyeichezea klabu hiyo ya London kwa miaka nane kabla ya uhamisho huo wa kushangaza, aliwasili kwa chakula cha jioni akiwa amevalia Sweater-shirt nyeusi iliyoandikwa Mickey Mouse, na jeans iliyopauka huku akiwa ametinga viatu vya kufanyia mazoezi mepesi(simpo).
Alikua ameongozana na mkewe na mama wa watoto wake wawili aitwaye Bouchra.
Bouchra mwenye umri wa miaka 28 alitinga skinny jeans iliyompendeza, top nyeusi yenye kola ya V, na jacketi jepesi la desaigner taupe suede kumachi rangi na viatu virefu (peep-toe heels).
No comments:
Post a Comment